Badilisha maelezo

Mteja anapaswa kusajiliwa kwa kutumia moja kati ya vitambulisho vilivyoidhinishwa na Mamlaka ya mawasiliano TCRA ambovyo ni Kiitambulisho cha Taifa, Kura, Pasport ya kusafiria, Leseni ya udereva na kitambulisho cha Mkaazi Zanzibar. Usalili utakaofanyika bila kutumia moja ya vitambulisho hivi si sahihi na mteja anashauriwa kutembelea maduka yetu yaliyo sehemu mbalimbali nchini kuhuisha/kubadili taarifa zake au tembelea tovuti http://halotel.co.tz:9003/web-portal/ kukamilisha usajili wako

Ukamilifu wa usajili unakuwezesha kumiliki laini yako na kukuwezesha kufurahia huduma maridhawa za Halotel

Zingatia: Namba yako ya simu ni utambulisho wako endapo tu imesajiliwa kwa taarifa sahihi