Wakala wa Halopesa

Jinsi ya kuwa wakala wa HaloPesa

Ni rasihi sana kuwa wakala wetu wa HaloPesa kwa kufuata haya yafuatayo:

-          Tembelea duka lolote la Halotel au Wasiliana na wakala wetu wakuu wa HaloPesa

-          Ambatanisha kopi zifuatazo:

1.    Leseni ya Biashare

2.    TIN namba

3.    Kopi ya kitambulisho

4.    Picha 2 za Passport size za hivi karibuni

5.    Kujaza fomu ya uwakala

6.    Mkataba wa Uwakala

 

Baada ya Kuwa Wakala wa HaloPesa

Hakikisha unayatekeleza haya baada ya kupata lini yako ya uwakala wa HaloPesa

1.    Bandika ada za wateja (customer Tariffs) katika eneo lako la Biashara

2.    Bandika stika ya wakala yenye namba yako ya uwakala

3.    Kuwa na kitabu cha kutunza kumbukumbu ya miamala (Logbook) na uorodheshe kila muamala utakaoufanya.

 

Faida ya kuwa wakala wa HaloPesa

-          Kamisheni nono kwa kila muamala utakaoufanya

-          Kutuma pesa mahali popote ndani ya Tanzania

-          Kukuza biashara yako kwa kuongeza wateja

-          Usalama wa pesa/floti ulizonazo

-          Kuweka floti kwa njia rahisi kabisa kupitia banki mbalimbali na mawakala wetu wakuu

 

Sehemu ya Kupata Floti

1.    Kupitia wakala wako mkuu

2.    Kwenye maduka yetu mbalimbali ya Halotel

3.    Kupitia bank (CRDB, ACB, UBA,TPB, PBZ,AZANIA BANK,FINCA)

 

Kwa msaada zaidi wasiliana na huduma kwa wateja kwa kupiga 100 au tembelea duka letu lolote lililokaribu nawe.