Tafadhali Nipigie

TAFADHALI NIPIGIE

Huduma inayokufanya uendelee kuwasiliana! Tafadhali nipigie ni njia ya haraka ya kuwasiliana na mtu wakati unapokuwa huna muda wa maongezi(salio) kwenye simu yako. 

Ni huduma inayokufanya utume meseji BURE kwa mtu unaetaka kuwasiliana nae wakati unapokuwa hauna muda wa maongezi  ili kuweza kupiga simu au kutuma SMS na inakusaidia pale unapokuwa na dharura.

Huduma inapatikana kwa njia ya SMS/USSD na STK.

 

Jinsi ya kutumia huduma 

Ni rahisi sana kujiunga na huduma hii, piga *140*(Namba ya Mpokeaji) #

SMS itatumwa kwa Yule mtu ikiwa na namba yako pamoja na  maneno “Tafadhali Nipigie”.

 

Gharama ya huduma 

Huduma ya Tafadhali nipigie ni BURE!