Muongozo wa haraka kutatua matatizo ya intaneti nyumbani
Ili WiFi iweze kufika umbali mrefu hakikisha unatumia WiFi kwenye maeneo yenye vizuizi vichache kama milango ya chuma, ukuta , vioo vitu vingine vinavyoweza kuzuia.
Badilisha mwelekeo wa antena ili Wi-Fi ifikie sehemu unayohitaji, au ongeza kifaa kingine cha Wi-Fi (“Mesh Wi-Fi” ni teknolojia nzuri kutatua tatizo hili).
Joto, unyevu, na vumbi vinaweza kufanya kifaa (router) kiache kufanya kazi Hakikisha kifaa kipo kwenye sehemu isiyo na joto (usikiweke juu ya TV, jikoni, jua, au sehemu zinazofanana), isiyo na unyevu (karibu na maji), na isiyo na vumbi.
Iwapo hauitaji kutumia kifaa kizime
Kama kuna watumiaji wengi wa intaneti yako unaweza kuboresha kifurushi cha huduma chenye speed kubwa zaidi, au badilisha pasword ya Wi-Fi kila baada ya miezi 2 ili watumiaji wa internet wapungue.
Iwapo kuna vifaa vingi vinavyotuma Wi-Fi tofauti karibu na kifaa chako katika eneo dogo, vinaweza kusababisha muingiliano wa mawimbi (interference) na hivyo kuathiri ubora wa intaneti yako.
Unaweza kukagua hali hiyo kwa kufungua sehemu ya Wi-Fi kwenye simu yako ya mkononi. Ukiangalia orodha ya mitandao inayopatikana, utaona Wi-Fi nyingi zenye nguvu zikionekana. Hii ni dalili kuwa eneo hilo lina msongamano wa mawimbi. Iwapo kuna Wi-Fi nyingi ni muhimu kutafuta njia ya kupanga upya Wi-Fi yako ili iwe na utulivu zaidi
Fuata hatua zilizotajwa hapo juu ili kukagua umeme, nyaya, mawimbi ya Wi-Fi, na hali ya kifaa chako.Itachukua dakika chache tu kurekebisha changamoto nyingi zinazojitokeza mara kwa mara.
Kama tatizo halijatatulika, tafadhali piga simu namba: 0623 100 100 kwa msaada wa haraka.











